Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 6 | Lands, Housing and Human Settlement Development | Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi | 89 | 2023-02-07 |
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kurasimisha, kupanga na kupima ardhi katika Miji Midogo ya Mawengi, Lugarawa, Luilo na Manda – Ludewa?
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba kujibu swali Na. 89 lililoulizwa na Mheshimiwa Joseph Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Wizara kupitia Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi iliikopesha Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kiasi cha shilingi milioni 405 kwa lengo la kupanga na kupima na kurasimisha miji midogo ya Mlangali, Mavanga, Ludewa na Mudindi ambapo jumla ya viwanja 7,911 vimepangwa na viwanja vingine 2,120 vimekamilika katika utaratibu.
Mheshimiwa Naibu Spika, natoa maelekezo wataalamu wa ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuanza kukusanya takwimu muhimu kwa ajili ya kupanga na kupima katika maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved