Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 6 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 94 | 2023-02-07 |
Name
Bernadeta Kasabago Mushashu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza: -
Je, Serikali ina mkakati gani wa kukomesha ukatili wa kijinsia nchini?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Bernadeta Kasabago Mushashu, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia unaozingatia kuimarisha uchumi wa kaya, kutokomeza mila na desturi zinachochea ukatili, kuimarisha malezi na makuzi na kusimamia sheria na kuwezesha huduma kwa waathirika.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto zimeundwa kuanzia ngazi ya Taifa hadi Kijiji. Zinafanya kazi zake katika Halmashauri kuhusu kutokomeza ukatili. Vituo vya Jeshi la Polisi, Magereza na Madawati ya Jinsia, Vyuo na Sehemu za Umma wanaunda madawati ya jinsia, Shule za Msingi na Sekondari zinaunda Madawati ya Ulinzi wa Watoto. Vilevile, Kampeni za kupinga ukatili zinaendelea sambamba na hatua za kuboresha sheria mbalimbali, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved