Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 6 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 100 | 2023-02-07 |
Name
Iddi Kassim Iddi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Msalala
Primary Question
MHE. IDDI K. IDDI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga majosho ya kuogesha mifugo katika Halmashauri ya Msalala?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, (Mb), kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali ilifanya ukarabati wa majosho matano (5) katika kata za Burige, Lunguya, Mega, Ntobo na Ngaya zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala. Aidha, Serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majosho katika halmashauri mbalimbali nchini; ikiwemo Halmashauri ya Msalala. Pia Serikali inaendelea kuhamasisha wafugaji kuchangia ujenzi wa miundombinu ya mifugo ikiwemo ujenzi wa majosho. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved