Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 7 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 111 | 2023-02-08 |
Name
Mwantumu Mzamili Zodo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MWANTUMU M. ZODO aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha Wakulima wa zao la Mwani ili kuongeza tija?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantumu Zodo, Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2022/2023 Serikali imetenga fedha za program maalum ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) kupitia dirisha la Extended Credit Facility (ECF) kwa ajili ya kuwawezesha wakulima wa mwani pembejeo kwa mkopo wa masharti nafuu na usio na riba kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha kwa awamu ya kwanza, Wizara itatoa pembejeo za mwani zenye thamani ya shilingi 447,251,244 kwa wakulima 343 waliokwenye vikundi katika wilaya saba za Muheza, Pangani, Mtama, Mkuranga, Kilwa, Lindi Mjini na Mtwara Vijijini, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved