Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 8 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 127 | 2023-02-09 |
Name
Dr. Jasson Samson Rweikiza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Kyatema – Kanazi – Ibwela – Katoro – Kyaka kwa kiwango cha lami?
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Jasson Samson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kyatema – Kanazi – Ibwela – Katoro – Kyaka yenye urefu wa kilometa 60.6 umekamilika mwezi Oktoba, 2022. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved