Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 9 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 136 2023-02-10

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: -

Je, ni chombo gani kinadhibiti vyuo binafsi vinavyodahili walimu nchini?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Idara ya Udhibiti Ubora wa Shule ndiyo yenye jukumu la kuthibiti ubora wa elimu inayotolewa katika vyuo vya ualimu vya binafsi nchini. Mamlaka haya ni kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 kifungu cha 25 na marekebisho yake kifungu cha 10 cha mwaka 1995.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa vyuo vikuu binafsi vinavyodahili walimu nchini, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ndio chombo chenye mamlaka ya kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa katika vyuo hivyo. Mamlaka haya ni kwa mujibu wa Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura Na. 346 ya Sheria za Tanzania, nakushukuru.