Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 9 Energy and Minerals Wizara ya Madini 140 2023-02-10

Name

Mrisho Mashaka Gambo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arusha Mjini

Primary Question

MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: -

Je, nini hatma ya madai ya maslahi ya waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa TanzaniteOne?

Name

Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Longido

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Madini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa Wizara ya Madini imepokea malalamiko ya kutolipwa mishahara ya waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited (TML) iliyokuwa ikichimba madini katika eneo la Kitalu ā€˜Cā€™ Mirerani.

Mheshimiwa Spika, Wizara ilifuatilia suala hili na kubaini kuwa wafanyakazi 540 walifungua shauri katika Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA) Arusha na shauri hilo Na. CMA/ARS/ARD/112/2018 ni la madai ya malimbikizo ya mishahara ya miezi 11 na stahiki zao zingine.

Mheshimiwa Waziri, shauri hilo lilisikilizwa na hukumu ilitolewa kuwa TML ilipe wafanyakazi hao jumla ya shilingi 2,529,331,585 kama malimbikizo ya mishahara yao ya miezi 11 na stahiki zao zingine.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hukumu kutolewa hadi sasa wafanyakazi hao hawajalipwa stahiki zao. Hata hivyo, kwa kuwa suala hili limesikilizwa na kutolewa maamuzi na Mahakama, na bado lipo kwenye taratibu za kisheria, Wizara ya Madini inasubiri taratibu za mahakama kukamilika ili kujua hatima ya suala hili, ahsante sana.