Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 11 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 91 | 2022-04-22 |
Name
Elibariki Emmanuel Kingu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Magharibi
Primary Question
MHE. ELIBARIKI I. KINGU aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga majosho ya mifugo katika Kata za Makilawa, Igelansoni, Iyumbu, Ighombwe, Mgungira na Mwaru Wilayani Ikungi?
Name
Mashimba Mashauri Ndaki
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Magharibi
Answer
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Elibariki Immanuel Kingu Mbunge wa Singida Magharibi kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/ 2022, Wizara inakamilisha ujenzi wa majosho 168 katika Halmashauri 80 kwa gharama ya shilingi bilioni 3.033. Aidha, kati ya majosho hayo, majosho mawili yanajengwa katika Kata za Mgungira na Siuyu katika Halmashauri ya Ikungi.
Mheshimiwa Spika, Wizara inatambua uhitaji mkubwa wa majosho katika maeneo mbalimbali nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara itaendelea na ujenzi wa majosho katika maeneo yenye uhitaji yakiwemo ya Jimbo la Ikungi. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved