Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 11 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 92 | 2022-04-22 |
Name
Ally Anyigulile Jumbe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyela
Primary Question
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza: -
Je, ni lini Barabara inayounganisha Wilaya ya Kyela na Ludewa kupitia Matema, Ikombe mpaka Liuli itaanza kujengwa?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFRY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ally Anyingulile Jumbe Mlaghila, Mbunge wa Kyela kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara inayounganisha Wilaya ya Kyela na Ludewa yenye urefu wa km 156 inapita kwenye safu ya milima ya Livingistone yenye miteremko mikali na miamba kubwa ya mawe.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza kufungua barabara hii kwa awamu kwa kufyeka misutu na kupasua miamba. Azma ya Serikali ni kuifungua barabara yote kuanzia Lupingu (Ludewa/ - Lumbila-Matema (Kyela).
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved