Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 19 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 170 | 2022-05-10 |
Name
Conchesta Leonce Rwamlaza
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Daraja la Kalebe – Bukoba Vijijini ili kuwezesha magari yenye uzito zaidi ya tani kumi kupita kwenye daraja hilo?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi ya kujenga Daraja la Kalebe ambapo kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja hili inaendelea chini ya Mkataba wa Usanifu wa Barabara ya Kyaka II – Kanazi – Kyetema. Kazi ya usanifu imepangwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu wa 2022.
Mheshimiwa Spika, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved