Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 21 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 187 2022-05-12

Name

Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. RITHA E. KABATI K.n.y. MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza: -


Je, ni lini Serikali itajenga daraja la Ugalla lililopo katika Kata ya Ugalla?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Nsimbo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa kina wa Daraja la Ugalla lenye urefu wa mita 150, ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa ujenzi. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha ili kuanza ujenzi wa daraja hilo. Ahsante.