Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 1 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 11 | 2023-04-04 |
Name
Nusrat Shaaban Hanje
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza: -
Je ni lini Serikali itatoa mikopo kwa wanafunzi wa Vyuo vya Kati nchini?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia naomba kujibu Swali la Mheshiwa Nusrat Shaaban Hanje, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa elimu ya kati katika maendeleo ya nchi, Serikali imeendelea kugharamia uendeshaji wa vyuo vya kati kupitia ruzuku ambapo kwa mwaka 2022/2023, imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 41.47 kwa wanafunzi 2,435 waliopo katika vyuo vya kati wanaosoma fani za sayansi na ufundi. Aidha, Serikali inakamilisha taratibu za kuwezesha mikopo kutolewa kwa ajili ya elimu ya kati.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved