Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 2 | Good Governance | Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) | 19 | 2023-04-05 |
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuzisaidia Kibajeti Taasisi za Wenza wa Viongozi Wakuu wa nchi ili ziweze kujiendesha na kupata ufadhili?
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ta Utumishi wa Umma na Utawala Bora naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abubakar Damian Asenga Mbunge wa Kilombero kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa sheria za nchi, taasisi za wenza wa viongozi wakuu wa nchi zinasajiliwa na kuendeshwa kwa taratibu zinazotumika kusajili na kuendesha taasisi nyingine binafsi na zisizo za Kiserikali. Hadi sasa Serikali haina mwongozo wa kisheria au kikanuni unaoielekeza kutoa usaidizi wa kibajeti kwa taasisi za wenza wa viongozi wakuu wa nchi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved