Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 2 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 23 | 2023-04-05 |
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Primary Question
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Daraja la Mto Lumpungu katika Jimbo la Muhambwe?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Mto Lumpungu unatenganisha nchi ya Burundi na Tanzania katika Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma kwenye Kijiji cha Kibuye, Kata ya Kumsenga. Kwa kuwa ujenzi wa daraja hili utahusisha nchi mbili Burundi na Tanzania, Serikali itaanzisha mazungumzo na nchi ya Burundi ili ziweze kukubaliana kuhusu ujenzi wa daraja hili, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved