Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 5 | Public Service Management | Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) | 56 | 2023-04-12 |
Name
Martha Festo Mariki
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya upungufu wa Watumishi katika Mkoa wa Katavi?
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Martha Mariki, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Katavi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi wa Mkoa wa Katavi kila mwaka kwa kuendelea kutenga Ikama na Bajeti kama inavyopitishwa na Bunge lako. Katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, Serikali ilitenga nafasi 522 za kada mbalimbali kwa Mkoa wa Katavi na katika mwaka wa fedha ujao (2023/2024) tunakusudia kutenga Ikama ya ajira mpya 914 kwa Mkoa wa Katavi iwapo Bunge lako likiridhia na kuipitisha Bajeti ya Serikali iliyopendekezwa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved