Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 6 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 74 2023-04-13

Name

Mrisho Mashaka Gambo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arusha Mjini

Primary Question

MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:-

Je, lini Wananchi wa Kata ya Moshono katika barabara ya mzunguko ya Kona ya Kiserian watalipwa fidia?

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi walioathirika na kupisha ujenzi wa barabara ya mzunguko (Arusha bypass) kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007.