Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 76 2023-04-13

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: -

Je, lini Miradi ya Umwagiliaji katika Vijiji vya Msange na Mnghamo – Singida Kaskazini itakamilika?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Ighondo Ramadhani Mbunge wa Singida Kaskazini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika mwaka wa fedha 2023/2024 imetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi wa Mughamo na kuanza ujenzi wa bwawa na miundombinu mingine ya umwagiliaji katika Skimu ya Msange.