Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 81 2023-04-14

Name

Anastazia James Wambura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA K.n.y. MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA aliuliza: -

Je, ni shule ngapi za sekondari zimejengwa katika Mkoa wa Mtwara ambao una zaidi ya kata 50 ambazo hazina shule?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anastazia James Wambura, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari imejenga shule 231 za kata na shule 10 za wasichana za kitaifa katika mikoa 10. Hii ikiwa ni awamu ya kwanza ya ujenzi kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari.

Mheshimiwa Spika, katika awamu hii ya kwanza Mkoa wa Mtwara umeshajengewa shule 10 za kata katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa wanafunzi na kata ambazo zilikuwa hazina shule.