Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 9 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 112 | 2023-04-18 |
Name
Ally Juma Makoa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kondoa Mjini
Primary Question
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza: -
Je, lini barabara ya kilometa 0.8 kutoka Benki ya NMB hadi National Milling Kondoa Mjini itajengwa kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Juma Makoa, Mbunge wa Kondoa Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika mwaka wa fedha 2023/2024 imepanga kuanza ujenzi wa barabara za Mji wa Kondoa kwa kiwango cha lami kwa urefu wa kilomita 3, ikiwemo kipande cha barabara ya kutoka Benki ya NMB hadi National Milling chenye urefu wa km 0.8. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved