Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 9 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 121 | 2023-04-18 |
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuamua kuwa wasichana wasiolewe chini ya miaka 18?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatvyo: -
Mheshimiwa Spika, Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 inatambua mtu mwenye umri chini ya miaka 18 kuwa ni mtoto, hivyo ni kosa la jinai kumuhusisha na mahusiano ya kimapenzi pia kumuozesha. Kwa upande mwingine Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inaruhusu mtoto wa kike kuingia kwenye ndoa akiwa na miaka 14. Hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeshakusanya maoni kutoka kwa wadau kuhusu upi ni umri sahihi wa kuoa na kuolewa.
Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa maoni hayo umeshakamilika na yatawasilishwa ndani ya Bunge ili yajadiliwe na mabadiliko kufanyika kadri Bunge litakavyoona inafaa ili kumlinda mtoto wa kike afikie ndoto zake. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved