Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 11 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 138 2023-04-20

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafufua upya Tume ya Taifa ya Mipango?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, naomba kujibu swali namba 138 lililoulizwa na Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya Muswada wa Sheria kuanzisha Tume ya Mipango. Muswada huu unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni katika Mkutano huu wa Kumi na Moja wa Bunge lako unaoendelea sasa. Muswada wa Sheria ukipitishwa Bungeni, Tume ya Mipango inatarajiwa kuanza shughuli zake katika mwaka wa fedha 2023/2024 yaani tarehe 1 Julai, 2023.