Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 11 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 140 2023-04-20

Name

Mussa Ramadhani Sima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mjini

Primary Question

MHE. FRANCIS I. MTINGA K.n.y. MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya mchepuko kutoka Kisaki – Unyamikumbi - Unyambwa hadi Mtipa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mussa Ramadhan Sima, Mbunge wa Singida Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali tayari imekamilisha Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa kina wa barabara ya mchepuko katika Mji wa Singida (Singida Bypass) kutoka Kisaki – Unyamikumbi – Unyambwa hadi Mtipa yenye urefu wa kilometa 46. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.