Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 12 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 157 2023-04-24

Name

Michael Constantino Mwakamo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Vijijini

Primary Question

MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kuwawekea mazingira mazuri Wakulima wadogo wa kilimo cha Umwagiliaji katika Mto Ruvu?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Michael Constantino Mwakamo, Mbunge wa Kibaha Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na hatua mbalimbali za kuboresha mazingira ya kilimo kwa wakulima wadogo ndani ya Bonde la Mto Ruvu kwa kubaini maeneo yanayofaa kwa ujenzi wa mabwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa Skimu ya Kisere (Nyani), usanifu huu ukikamilika ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji utaanza katika Mwaka wa Fedha 2024/2025.