Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 13 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 174 | 2023-04-25 |
Name
Maulid Saleh Ali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Welezo
Primary Question
MHE. MAULID SALEH ALI aliuliza: -
Je, kuna mkakati gani wa kudhibiti utapeli unaofanywa kwa kutumia namba za simu za nje?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maulid Saleh Ali, Mbunge wa Jimbo la Welezo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, utapeli ama kwa lugha nyingine ni udanganyifu unaofanywa kwa kutumia simu za nje hudhibitiwa kwa kushirikisha Mamlaka za Udhibiti kwenye nchi ambako namba zinazotumika zimegawiwa. Mamlaka hizo huchukua hatua stahiki kwa kadri wanavyopokea taarifa zinazohusiana na utapeli huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni Mwanachama wa Jumuiya za Kikanda na Kimataifa kama vile ATU, EACO, CRASA, CTO, ITU, UPU, PAPU na kadhalika. Ushirikiano uliopo kupitia Jumuiya hizi husaidia sana kwenye utatuzi wa masuala mengi yakiwemo yanayohusu utapeli unaofanyika kwenye mitandao ya simu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved