Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 16 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu | 198 | 2023-05-02 |
Name
Kiswaga Boniventura Destery
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Magu
Primary Question
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali italipa kiinua mgongo kwa wazee ambao hawajawahi kuajiriwa?
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kiinua mgongo ni malipo ambayo hulipwa na mwajiri pindi mfanyakazi wake anapostaafu kufanya kazi. Hata hivyo, kutokana na kuwepo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambapo mwajiriwa na mwajiri huchangia, mfanyakazi hulipwa pensheni badala ya kiinua mgongo na hupokea mafao ya mkupuo mara anapostaafu na badaye kuendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi kwa maisha yake yote. Hivyo, kwa sasa hakuna mfumo wa kulipa kiinua mgongo kwa mzee ambaye hajawahi kuajiriwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved