Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 16 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 201 | 2023-05-02 |
Name
Esther Lukago Midimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kurudia ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi – Maswa ambayo imejengwa chini ya kiwango na imeshaharibika?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Lukago Midimu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, mkandarasi alianza kazi za kurudia ujenzi wa maeneo yote ambayo yalionekana hayakidhi viwango vya ujenzi kwa gharama zake mwenyewe mnamo tarehe 10 Juni, 2021. Kazi za marudio ziko katika hatua za mwisho ambapo zimefikia asilimia 98 na zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei, 2023.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved