Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 16 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 203 | 2023-05-02 |
Name
Zuena Athumani Bushiri
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: -
Je, ni lini umeme utafungwa kwenye mnara wa halotel uliopo kata ya Ngujini Wilayani Mwanga?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuena Athumani Bushiri Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Jukumu la kuunganisha umeme kwenye minara ya mawasiliano ya simu nchini, ikiwemo ile iliyojengwa kwa ruzuku ya Serikali, ni jukumu la watoa Huduma, hii ni pamoja na gharama za kuunganisha umeme na kuendesha minara husika.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kusimamia huduma za mawasiliano nchini kwa kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi matakwa ya leseni zinazotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved