Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 20 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 261 | 2023-05-08 |
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZAINAB A. KATIMBA aliuliza: -
Je lini Serikali itaanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya kada ya kati?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na taratibu za maandalizi ya kuwezesha utoaji wa mikopo kwa elimu ya kati ikiwemo utafutaji wa vyanzo endelevu vya ugharamiaji wa elimu na mafunzo nchini. Aidha, kwa kutambua umuhimu wa elimu ya kati katika maendeleo ya nchi, Serikali imeendelea kugharamia uendeshaji wa vyuo vya kati kupitia ruzuku ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023, imetenga kiasi cha shilingi bilioni 41.47 kwa wanafunzi 2,435 waliopo katika vyuo vya kati wanaosoma fani za sayansi na ufundi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved