Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 22 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 289 | 2023-05-10 |
Name
Florent Laurent Kyombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkenge
Primary Question
MHE. FROLENT L. KYOMBO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaongeza minara au kuboresha mawasiliano katika kata zote 20 za Wilaya ya Misenyi?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA NA HABARI, alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Frolent Laurent Kyombo Mbunge wa Nkenge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imetekeleza miradi ya mawasiliano iliyokamilika katika kata 10 za Wilaya ya Missenyi. Kufikia mwezi Machi, 2023 tayari ujenzi wa minara 13 imekamilika na inatoa huduma katika teknolojia ya 2G na 3G.
Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali Serikali imeshapata watoa huduma wa kufikisha huduma za mawasilioano katika Kata za Bugorora, Kasambya, Mutukula na Kakunyu ambapo tayari zimeshapata watoa huduma, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved