Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 23 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 296 | 2023-05-11 |
Name
Hassan Seleman Mtenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtwara Mjini
Primary Question
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja la Kilambo?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hasan Seleman Mtenga, Mbunge wa Mtwara Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Daraja la Kilambo linalopendekezwa kujenga litaunganisha Nchi ya Tanzania na Msumbiji katika Barabara ya Mangamba – Madimba – Tangazo – Kilambo yenye kilometa 36.8 Mkoani Mtwara. Kwa kuwa ujenzi wa daraja hili utahusisha Nchi mbili za Tanzania na Msumbiji, Serikali tayari imeanza mazungumzo ya awali na Nchi ya Msumbiji ili ziweze kukubaliana kuhusu ujenzi wa daraja hilo, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved