Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 24 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 312 2023-05-12

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza: -

Je, kuna mkakati gani wa kukomesha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). Ambapo, kamati za ulinzi wa wanawake na watoto zimeundwa kuanzia vijijini, mitaa hadi Taifa. Madawati ya jinsia na watoto sasa yako vituo vyote vya polisi. Madawati ya ulinzi na usalama wa watoto yanaendelea kuundwa ndani na nje ya shule zote za msingi na sekondari. Vyuo vyote vimeundwa madawati ya jinsia na mabaraza ya watoto 560 yameanzishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuimarisha utekelezaji wa MTAKUWWA, Serikali imeelekeza halmashauri zote kuhakikisha, ajenda ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto ni ya kudumu kwenye vikao ngazi zote, ahsante.