Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 25 | Lands, Housing and Human Settlement Development | Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi | 326 | 2023-05-15 |
Name
Emmanuel Peter Cherehani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Primary Question
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa nyumba za Watumishi nchini hasa katika Halmashauri mpya?
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Peter Cherehani, Mbunge wa Ushetu kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2012 hadi 2014, Serikali kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilijenga nyumba za gharama nafuu 1,189 katika halmashauri 31 kwa ajili ya kuziuza kwa watumishi waliopo katika Halmashauri hizo. Aidha, kuanzia mwaka 2013 hadi sasa, jumla ya nyumba 983 zimejengwa na taasisi ya Watumishi Housing Company katika mikoa 19 na kuuzwa kwa watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo Shirika la Nyumba la Taifa na Watumishi Housing itaendelea kujenga nyumba bora kwa ajili ya watumishi wa umma ili kuwaongezea tija katika utendaji kazi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved