Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 25 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 330 | 2023-05-15 |
Name
Eng. Stella Martin Manyanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nyasa
Primary Question
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza: -
Je, lini Mahakama ya Wilaya ya Nyasa itaanza kujengwa?
Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, nikushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria naomba sasa nijibu swali la Mheshimiwa Engineer Stella Martin Manyanya, Mbunge wa Nyasa kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kujenga Mahakama ya Wilaya ya Nyasa katika mwaka huu wa fedha wa 2022/2023, ambapo taratibu zote za awali za kupitia michoro na makadirio ya gharama zimekamilika, na hatua za kupata mkandarasi wa ujenzi ipo katika hatua za mwisho.
Mheshimiwa Spika, Tunategemea muda wowote jengo hili litaanza kujengwa, na kukamilika katika mwaka ujao wa fedha wa 2023/2024.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved