Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 26 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 344 2023-05-16

Name

Esther Edwin Maleko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha Uwanja wa Ushirika Moshi ili kukuza utalii wa michezo nchini?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Edwin Maleko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kinamiliki viwanja mbalimbali vya michezo ambavyo ni uwanja wa mpira wa miguu, pete, wavu, kikapu na riadha. Viwanja hivyo ni miongoni mwa miundombinu iliyojengwa na Serikali ili kuendeleza michezo na burudani kwa jumuiya ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi na wadau wengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa viwanja hivyo vipo katika hali nzuri na vinaendelea kutumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa. Aidha, Chuo kina utaratibu wa kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa viwanja hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.