Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 28 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 369 2023-05-18

Name

Shamsia Aziz Mtamba

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y. MHE. SHAMSIA A. MTAMBA aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara inayotoka Mtwara Mjini kuelekea Msimbati?

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Shamsia Azizi Mtamba, Mbunge wa Mtwara Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, barabara inayotoka Mtwara Mjini mpaka Msimbati ni barabara ya Mangamba – Madimba hadi Msimbati yenye urefu wa kilometa 35.63 inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii imekamilika. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.