Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 32 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu | 415 | 2023-05-24 |
Name
Hawa Mchafu Chakoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza: -
Je, Serikali imefikia wapi kuhusu mchakato wa pensheni kwa wazee wote?
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, pensheni kwa wazee wote inajumuisha wazee ambao walikuwa katika ajira ambao kwa sasa wanalipwa pensheni na Mifuko waliyochangia wakati wanafanya kazi na pili, wazee ambao hawajawahi kuajiriwa kwa sasa hawalipwi.
Mheshimiwa Spika, mchakato wa kuwalipa pensheni wazee wote ambapo utajumuisha wazee ambao hawajawahi kuajiriwa ni utaratibu mpya ambao utahitaji kugharamiwa na bajeti ya Serikali. Hivyo, itahitaji kufanyika utafiti wa kina ili kuona uwezo wa Serikali katika kulipa pensheni kwa wazee wote. Hata hivyo, kwa sasa Serikali imekuwa inahudumia wazee kutoka katika familia au kaya zenye umaskini uliokithiri kupitia Mradi wa TASAF ambapo wazee ni sehemu ya familia hizo, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved