Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 1 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 14 | 2023-08-29 |
Name
Abdallah Dadi Chikota
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Primary Question
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza: -
Je, ni lini kutakuwa na kiuatilifu kimoja cha magonjwa kwenye zao la korosho?
Name
Anthony Peter Mavunde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Nanyamba kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika zao la korosho kuna magonjwa makuu manne ya ubwiriunga, blaiti, chule na debeki yanayodhibitiwa kwa viuatilifu vyenye viambata amilifu tofauti.
Mheshimiwa Spika, ili kuongeza ufanisi wa udhibiti wa visumbufu vya mazao, Serikali itaendelea kuimarisha utafiti na kushauri wakulima kutumia viuatilifu vyenye tija zaidi katika kilimo. Aidha, Serikali kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu inaendelea kupitia upya usajili wa viuatilifu vyote ili kubaki na viuatilifu vinavyofaa sokoni kulingana na aina ya zao, eneo na magonjwa yaliyopo.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved