Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 2 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 32 | 2023-08-30 |
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: -
Je, lini Serikali itafufua kilimo cha pamba katika Wilaya ya Kilwa?
Name
Anthony Peter Mavunde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa maeneo yaliyo chini ya karantini ya pamba katika eneo la kusini mwa Tanzania kutokana na uwepo au kupakana na nchi zilizoathiriwa na funza mwekundu (diparopsis castenea) ambaye ni mdudu hatari wa zao la pamba.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2020/2021 Serikali ilifanya tathmini ya hali ya funza mwekundu na kubaini kuwa mdudu huyo bado yupo katika maeneo ya karantini. Aidha, Wizara itaendelea kufanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi za Kimataifa kuhusu namna bora ya kudhibiti mdudu huyo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved