Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 2 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 33 | 2023-08-30 |
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:-
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha inapata data za bidhaa zote za kilimo zinazosafirishwa nje ya nchi?
Name
Anthony Peter Mavunde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Grace Victor Tendega, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaendelea kuboresha mfumo wa Agricultural Trade Management Information System (ATMIS) kwa ajili ya kuufungamanisha na mfumo wa pamoja wa forodha wa Tanzania (Tanzania Custom Intergrated Systems - TANCIS) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kufunganishwa kwa mfumo wa ATMIS na TANCIS kutaboresha upatikanaji wa takwimu za mazao na bidhaa za kilimo zinazoingizwa au zinazosafirishwa nje ya nchi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved