Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 2 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 37 | 2023-08-30 |
Name
Martha Nehemia Gwau
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARTHA N. GWAU aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za kuwahifadhi waliofanyiwa ukatili ikizingatiwa kuwa ukatili kwa watoto na wanawake umeongezeka?
Name
Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Martha Nehemia Gwau, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu mpango wa kuwahifadhi waliofanyiwa ukatili (kujenga nyumba za kuwahifadhi waliofanyiwa ukatili), Serikali imeandaa Mwongozo wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Nyumba Salama wa Mwaka 2019, kwa ajili ya manusura wa vitendo vya ukatili pamoja na wahanga wa biashara haramu wa usafirishaji wa binadamu. Lengo ni kuweka mazingira wezeshi kwa uanzishaji huduma ya nyumba salama kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na kwa watoto hapa nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, Hadi kufikia June 2023 jumla ya nyumba salama 12 zimeanzishwa na kusajiliwa katika Mikoa ya Arusha, Kigoma, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza. Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kuhakikisha upatikanaji endelevu wa huduma hii kwa mujibu wa Mwongozo wa mwaka 2019.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved