Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 440 2023-05-26

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. ISSA J. MTEMVU K.n.y. MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: -

Je, ni lini Mradi wa DMDP Awamu ya Pili utaanza kwa lengo la kutatua changamoto ya miundombinu Kigamboni?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa DMDP Awamu ya Pili kupitia mkopo wa Benki ya Dunia unatarajiwa kuanza mwezi Februari, 2024 na utahusisha ujenzi wa miundombinu ya barabara, mifereji ya maji ya mvua pamoja na madaraja. Kwa sasa mradi upo katika hatua ya upembuzi yakinifu na usanifu. Hatua hiyo itakapokamilika, ombi la fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo litawasilishwa Benki ya Dunia.