Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 5 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 64 | 2023-09-04 |
Name
Kasalali Emmanuel Mageni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sumve
Primary Question
MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza: -
Je, lini Serikali itahakikisha tatizo la kutokuwepo mawasiliano ya simu ya uhakika katika maeneo mengi ya Jimbo la Sumve linatatuliwa?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kasasali Emmanuel Mageni, Mbunge wa Jimbo la Sumve kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imefikisha huduma za mawasiliano katika Kata za Bugando, Lyoma, Mwandu, Ngulla na Sumve.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali itafanya tathmini katika Jimbo la Sumve ili kubaini maeneo ambayo bado yana changamoto za upatikanaji wa huduma za mawasiliano ili yatafutiwe fedha kwa ajili ya kutatua changamoto hizo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved