Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 5 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 72 | 2023-09-04 |
Name
Godwin Emmanuel Kunambi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mlimba
Primary Question
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani kuhusu ujenzi wa barabara ya Mafinga hadi Mlimba?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, nami kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako kama Naibu Waziri wa Ujenzi, naomba nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, maana ametoa kibali hiki. Nichukue fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini ili niweze kumsaidia katika nafasi ya Unaibu Waziri wa Ujenzi, pia nikuahidi kwamba nitatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge lako Tukufu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba sasa nijibu swali. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Godwin Emmanuel Kunambi, Mbunge wa Mlimba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara inayoanzia Mafinga, eneo la Kinyanambo āCā hadi Kihansi (Mlimba) yenye urefu wa kilometa 126.39, ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya milioni 250 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Baada ya kukamilika usanifu na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved