Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 36 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 474 2023-05-30

Name

Venant Daud Protas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igalula

Primary Question

MHE. VENANT D. PROTAS aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Jimbo la Igalula?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Venant Daud Protas Mbunge wa Jimbo la Igalula kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa vyuo vya ufundi stadi katika kuwasaidia wananchi kupata ujuzi utakao wasaidia kutekeleza kazi zao za kiuchumi. Kwa sasa Serikali inatekeleza azma ya kujenga chuo cha ufundi stadi katika kila mkoa na wilaya nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Igalula lipo katika Wilaya ya Uyui na kwa sasa Serikali inakamilisha ujenzi wa Chuo cha Wilaya ya Uyui. Ujenzi huo umefikia asilimia 97 na chuo hiki kimeshaanza kutoa mafunzo ya muda mfupi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukamilisha ujenzi wa vyuo vya VETA katika wilaya zote nchini, Serikali itaangalia uwezekano wa kujenga vyuo vya VETA katika ngazi za majimbo na ngazi zingine za chini kadri ya upatikanaji wa fedha na uhitaji, nakushukuru.