Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 39 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 503 2023-06-02

Name

Rehema Juma Migilla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:-

Je, lini Serikali itawapa ajira za kudumu walimu walioajiriwa tangu mwaka 2002 kwa masharti ya ajira za muda Ulyankulu?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rehema Juma Migilla, Mbunge wa Jimbo la Ulyankulu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha 2017 – 2021 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua iliidhinishiwa na kuajiri walimu 13 ambao walitimiza sifa za kuajiriwa kwa masharti ya Ajira ya Kudumu na Malipo ya Uzeeni. Aidha, Walimu 29 wameajiriwa kwa masharti ya Ajira za Mkataba kwa kuwa walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 45. Walimu hawa walikuwa ni wakimbizi waliopatiwa uraia wa Tanzania baada ya kupata sifa kwa mujibu wa sheria.