Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 39 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 510 2023-06-02

Name

Omar Ali Omar

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Wete

Primary Question

MHE. OMAR ALI OMAR aliuliza: -

Je, kwa nini Serikali haipangi kusahihishia mitihani ya kidato cha nne Zanzibar?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omari Ali Omari, Mbunge wa Wete, kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2021 na 2022 Serikali ilisahihisha mitihani ya Taifa, kidato cha nne (CSEE) katika kituo cha Shule ya Sekondari Hasnuu Makame, Kusini Unguja. Aidha, Serikali itaendelea kusahihisha mitihani Zanzibar kwa vituo vya mitihani vyenye sifa za kulaza watahini wasiopungua 500 kwa wakati mmoja, kuwa na vyumba visivyopungua ishirini vya kazi, na miundombinu ya maji na umeme kwa wakati wote wa kazi ya kusahihisha, nakushukuru sana.