Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 39 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 511 2023-06-02

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:-

Je, ni ni kwa nini Serikali pindi inapotwaa maeneo ya wakulima isiwatengee maeneo mengine mbali ya kulipa fidia?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Naghenjwa Livingston Kaboyoka Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi, Sura 113 kifungu cha 3 Kifungu kidogo cha (1)(g), malipo ya fidia ni takwa la kisheria pindi Serikali inapotwaa ardhi kutoka kwa wananchi. Kimsingi, fidia kwa mujibu wa Sheria inajumuisha thamani ya ardhi na maendelezo yaliyopo juu ya ardhi. Fidia yaweza kulipwa kwa fedha au kupewa ardhi mbadala au vyote kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikitekeleza fidia ya ardhi mbadala au fedha au vyote kwa pamoja kutokana na mazingira ya eneo la mradi, ahsante.