Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 44 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 570 2023-06-09

Name

Emmanuel Lekishon Shangai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Primary Question

MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano katika Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Lekishon Shangai, Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ilifanya tathmini na kubaini changamoto ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na imekwisha wapata watoa huduma watakaofikisha huduma za mawasiliano katika Kata za Alailelai, Alaitolei, Engaresero, Mundarara, Ngoile, Olbalbal na Ololosokwan. Aidha, Serikali itayaingiza maeneo mengine yaliyobaki yenye changamoto ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika orodha ya miradi itakayotekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha. (Makofi)