Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 44 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 571 2023-06-09

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati kwenye Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kibondo pamoja na nyumba za Askari Polisi?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kibondo pamoja na nyumba za makazi ya Maofisa na Askari ni chakavu. Tathmini ya uchakavu kwa ajili ya kufanya ukarabati imefanyika na kiasi cha Sh.28,914,250/= kinahitajika kwa ajili ya kukarabati Kituo cha Polisi na Sh.109,288,000/= zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa nyumba nane za makazi ya Maofisa na Askari Polisi. Kulingana na hali ya upatikanaji wa fedha, Serikali imepanga kutekeleza ukarabati huo katika mwaka wa fedha 2024/2025, nakushukuru.