Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 46 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 586 2023-06-12

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza:-

Je, lini Serikali itatunga Sera ya Ugatuaji wa Madaraka na kutunga sheria ili kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mtaa?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Mohamed Kassinge, Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha maandalizi ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ambapo wadau mbalimbali wameshirikishwa na kutoa maoni yao. Aidha, Rasimu hiyo imewasilishwa katika ngazi ya maamuzi kwa mapitio na maelekezo zaidi.